Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 25 Aprili 2016 08:45

Tz: Miundombinu ndiyo chachu ya mradi wa mafuta

Tz: Miundombinu ndiyo chachu ya mradi wa mafuta

Waziri wa Nishati na Madini nchini Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa, miundombinu ya Tanzania na usalama ni moja ya mambo yaliyowezesha Tanzania kukabidhiwa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi bandari ya Tanga, Tanzania.

Muhongo ameyasema hayo, wakati akizungumza na waandishi wa habari mara tu baada ya kuwasili kutoka Kampala, Uganda na kuongeza kuwa, maunganiko ya reli ya Tanga hadi reli ya kati na pia uepo wa barabara, ndiko kulikoipatia Tanzania nafasi ya ujenzi wa bomba hilo kwani kaskazini mwa Kenya miundombinu hiyo haipo. Aidha Waziri Muhongo amemsifu Rais John Magufuli kwa kazi yake nzuri ya kusimamia ujenzi wa barabara wakati alipokuwa Waziri wa Ujenzi, na kusema, kama kungelikosekana miundombinu hiyo basi Tanzania haingepata fursa ya kupewa mradi huo muhimu Afrika Mashariki. Itafahamika kuwa, Tanzania ilikuwa ikishindana na Kenya katika kupata nafasi ya kutekeleza mradi huo wenye kilomita 1,403 utakaobeba mafuta ghafi kutoka eneo la Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga. Mradi huo unaokadiriwa kuwa wa thamani ya dola bilioni nne za Marekani ambazo ni sawa na Shilingi trilioni nane 8.7 umetajwa na serikali ya Tanzania kuwa ushindi mkubwa kwa nchi hiyo. Kabla ya hapo serikali ya Dar es Salaam, ilipeleka Uganda timu yake ya wataalamu ili kutetea ni kwa nini bomba hilo la mafuta linafaa kupitia Tanzania.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …