Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 24 Aprili 2016 19:19

Rais Kabila wa DRC aonana na Katibu Mkuu wa UN

Rais Kabila wa DRC aonana na Katibu Mkuu wa UN

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameonana na Ban Ki mooon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kujadiliana naye hali ya kisiasa na kiusalama ya nchi hiyo.

Shirika la habari la Xinhua limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Ban Ki moon na Joseph Kabila wameonana mjini New York Marekani na kujadiliana masuala yanayohusiana na kazi za kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo, maarufu kwa jina la Monusco.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka serikali ya Kongo kuchukua hatua zinazotakiwa kwa ajili ya kupunguza machafuko na hali ya wasiwasi na kuandaa mazingira mazuri ya kufanyika uchaguzi wa rais na bunge kwa usalama na amani.

Mazungumzo hayo yamefanyika wiki tatu baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupasisha azimio nambari 2277 kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kupitia azimio hilo lililopasishwa tarehe 31 Machi, Baraza la Usalama limemtaka Rais Joseph Kabila kuhakikisha kuwa uchaguzi wa rais unafanyika katika muda uliopangwa.

Azimio hilo aidha limewataka watu wote wanaohusika na masuala ya Kongo wasaidie juhudi za kuhakikisha kuwa uchaguzi huo unafanyika kiuadilifu na kutimiza viwango vyote vya kimataifa.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …