Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 23 Aprili 2016 08:51

UNHCR: Warundi wanazidi kuikimbia nchi yao

UNHCR: Warundi wanazidi kuikimbia nchi yao

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi (UNHCR), limetangaza kuwa idadi ya wakimbizi wa Burundi wanaoomba hifadhi nchi jirani inaongezeka na sasa imefikia 260,000.

Taarifa ya UNCHR imebaini kuwa mwaka mmoja tangu kuzuka kwa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, raia wa nchi hiyo wangali wanaendelea kuikimbia nchi hiyo kutokana na hofu ya vita na machafuko.

Taarifa ya UNHCR inasema kuwa ikiwa suluhisho la kisiasa halitapatikana nchini Burundi maelfu zaidi ya wakimbizi wanatarajiwa kuelekea nchi jirani. Aidha taarifa hiyo imesema wakimbizi wengi wanasimulia kutendewa vitendo vilivyo kinyume na haki za binadamu ikiwemo kuuwawa na mateso.

Shirika hilo limeitaka jamii ya kimataifa kusaidia katika kadhia hiyo hususan katika majadiliano jumuishi ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Burundi.

UNHCR hata hivyo imefafanua kuwa, katika siku za usoni wakati wa kurejea kwa wakimbizi nchini humo, itawekeza kutoa elimu kwa watoto na vijana, na kuwahamasisha wakimbizi kujitegemea kutokana na upungufu wa ufadhili wa fedha. Miongoni mwa nchi jirani zinazobeba mzigo mkubwa wa wakimbizi wa Burundi ni Tanzania.

Zaidi ya watu 400 wameripotiwa kuuawa na wengine karibu laki mbili na 60 elfu wamekuwa wakimbizi tangu mwezi Aprili mwaka jana wakati Burundi ilipotumbukia kwenye machafuko yaliyotokana na Rais Pierre Nkurunziza kuamua kugombea tena urais nchini humo. Wapinzani walisema hatua ya Nkurunziza kugombea urais muhula wa tatu mfululizo ni kinyume cha katiba ya nchi hiyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …