Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 22 Aprili 2016 12:17

Watu 7 wauawa katika mlipuko wa bomu Libya

Watu 7 wauawa katika mlipuko wa bomu Libya

Watu 7 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea katika mji wa Darnah, nchini Libya.

Mlipuko huo ulitokea jana katika eneo la al-Fataaih, ambapo watu saba waliuawa na wengine 13 kujeruhiwa. Shambulio hilo limetokea wakati ambao wakazi wa mji wa Darnah walioikimbia miji yao baada ya kuvamiwa na wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, kuanza kurejea makwao. Siku chache zilizopita, jeshi la Libya lilifanya operesheni kadhaa za kijeshi na kufanikiwa kuwatimua wanachama wa genge hilo.

Afisa mmoja wa serikali ambaye hakutaka kutaja jina lake amenukuliwa akisema kuwa, baada ya harakati ya vijana na Baraza la Mujahidina la mjini Darnah kuwafurusha wanachama wa Daesh mjini hapo, walidhibiti maeneo muhimu ya Kurfat Sab'a na al-Fataaih, huku wakiondoa vizuizi vyote vilivyowekwa na wapiganaji wa Daesh mjini hapo, suala ambalo liliwafanya wakazi wa maeneo hayo kuanza kurejea makwao.

Shambulio hilo linalotajwa kufanywa na Daesh, limefanyika kwa lengo la kuwazuia raia wa maeneo hayo kushindwa kurejea katika makazi yao. Tayari serikali mpya ya nchi hiyo, imesifu juhudi za wapiganaji wa serikali kufanikiwa kuyasafisha maeneo ya Darnah dhidi ya wanamgambo wa kigaidi.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …