Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 12 Aprili 2016 20:56

Boko Haram wanatumia watoto katika hujuma za kigaidi

Boko Haram wanatumia watoto katika hujuma za kigaidi
Kundi la magaidi wakufurishaji wa Boko Haram nchini Nigeria wanazidi kuwatumia watoto wadogo kusheheni bomu na kujiripua katika hujuma za kigaidi.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Watoto (UNICEF), katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita Boko Haram wameongeza mara 11 idadi ya watoto wanaotumiwa kutekeleza hujuma za kigaidi nchini Nigeria na pia katika nchi jirani za Cameroon, Chad na Nigeria. UNICEF imesema mwaka 2015 watoto 44 walitumiwa na Boko Haram kutekeleza hujuma za kigaidi ikilinganishwa na watoto wanne mwaka 2014.

Katika ripoti hiyo iliyotangazwa leo Jumanne, UNICEF imesema kulikuwa na mtoto moja kati ya kila magaidi watano wa Boko Haram waliojiripua. Aidha ripoti hiyo imesema wasichana ni asilimia 75 ya watoto waliotumia kutekeleza hujuma za kigaidi.

Mkurugenzi wa UNICEF magharibi na kati mwa Afrika, Manuel Fontaine, amesema watoto hao wanaotumia na Boko Haram ni waathirika na wala si wahalifu. Ameongeza kuwa watoto wanahadaiwa na kulazimishwa kufanya mashambulizi ya kigaidi huko Nigeria na katika nchi jirani.

Itakumbukwa kuwa Aprili mwaka 2014 magaidi wa Boko Haram waliwateka nyara wasichana 276 kutoka shule yao ya bweni katika mji wa Chibok katika jimbo la Borno ambalo ni ngome ya magaidi hao wa kitakfiri huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Wasichana kadhaa walitoroka lakini wengine 219 hawajulikani waliko.

Neno Boko Haram kwa lugha ya Kihausa lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram ambalo lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi hiyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …