Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 12 Aprili 2016 11:16

Iweje mauaji dhidi ya Waislamu Nigeria yameachwa?

Iweje mauaji dhidi ya Waislamu Nigeria yameachwa?

Mwanaharakati mmoja maarufu wa nchini Uingereza amekosoa vikali ukimya wa jamii ya kimataifa juu ya mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu nchini Nigeria.

Masudi Shajarah mkuu wa kamisheni ya haki za binaadamu ya Kiislamu nchini Uingereza aliyasema hayo hapo jana katika mahojiano na kanali ya Press Tv mjini London, Uingereza na kuongeza kuwa, ni miezi kadhaa sasa imepita tangu kujiri mauaji ya halaiki dhidi ya Waislamu nchini Nigeria huku jinai hizo zikiwa hazijachunguzwa. Shajarah ameongeza kuwa, ni suala la dharura kufuatiliwa wahusika wa jinai hizo na kupandishwa kizimbani. Itakumbukwa kuwa mwezi Disemba mwaka jana jeshi la Nigeria lilishambulia makazi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, kiongozi wa harakati ya Kiislamu ya nchini humo. Katika hujuma hiyo iliyojiri katika mji wa Zaria, jimbo la Kaduna kaskazini mwa nchi hiyo, jeshi la Nigeria liliwaua mamia ya Waislamu katika eneo hilo na kisha kuizika miili ya wahanga hao katika kaburi la umati. Licha ya mashirika mbalimbali likiwemo Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty Internationa, kuthibitisha jinai hiyo na kufichua kaburi hilo la umati, lakini hadi sasa bado hakujachukuliwa hatua zozote kimataifa kuhusiana na mauaji hayo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …