Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 11 Aprili 2016 17:49

Wapinzani DRC waliunga mkono azimio la UNSC

Wapinzani DRC waliunga mkono azimio la UNSC

Wapinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamesema kuwa, wanaunga mkono azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kufanyike uchaguzi wa nchi hiyo katika muda uliopangwa.

Olivier Kamitatu, mmoja wa wajumbe wa kundi la G7 linaloundwa na vyama sita vya kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amesema kuwa, serikali ya Kinshasa inapaswa kuheshimu azimio hilo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ufanyike katika muda uliopangwa.

Msimamo huo wa wapinzani wa serikali unakuja kufuatia matamshi ya Raymond Tshibanda, Waziri wa Mashauri ya Kigeni na Lambert Mende Omalanga Waziri wa Nawasiliano ambao wamesema kuwa, azimio hilo la Baraza la Usalama litashadidisha utumiaji mabavu na machafuko katika nchi hiyo.

Ikumbukwe kuwa, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitangaza mwezi Februari mwaka jana kuwa, uchaguzi wa rais na bunge wa nchi hiyo utafanyika Novemba 27 mwaka huu.

Hata hivyo wapinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema kuwa, kumekuwa na harakati zinazofanywa na chama cha Rais Joseph Kabila za kuakhirisha uchaguzi huo ili kiongozi huyo aendelee kubakia madarakani.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …