Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 10 Aprili 2016 19:41

‘Marekani imewatumia silaha magaidi wa ISIS Iraq’

‘Marekani imewatumia silaha magaidi wa ISIS Iraq’

Maafisa wa polisi nchini Iraq wanasema wameona ndege za kijeshi za Marekani zikiwateremeshia shehena za silaha magaidi wa ISIS au Daesh katika mkoa wa Al Anbar.

Katika mkanda wa video uliosambazwa na mtandao wa al-Maalomah leo Jumapili, askari hao wa Iraq wanasikika wakisema ndege ya Marekani ilionekana saa kumi alfajiri siku ya Ijumaa katika kisiwa cha Hadisah mkoani Al Anbar ikiwateremshia shehena ya silaha magaidi wa Daesh.

Askari mmoja anasikika akisema kuwa ndege hiyo ya Marekani ilivuruga mawasiliano ya polisi katika kisiwa cha Hadisah ili kuwazuia kuwasiliana na makao yao makuu.

Afisa wa polisi Muiraqi amesikika akisema, gari la magaidi wa ISIS iliwasilia eneo hilo dakika chache baadaye na kuchukua silaha hizo.

Hivi karibuni pia tovuti ya moonofalabama.org ilifichua kuwa, katika miezi ya hivi karibuni Marekani imetoa msaada wa tani elfu tatu za silaha kwa magaidi wa Al Qaeda na washirika wao nchini Syria.

Kwa muda mrefu sasa serikali ya Syria imekuwa ikisisitiza kuwa magaidi katika eneo hili wanapata misaada ya kifedha na kisilaha kutoka kwa nchi za Magharibi hasa Marekani na waitifaki wake wa eneo hili ambao ni Saudi Arabia, Qatar, Uturuki na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …