Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 09 Aprili 2016 20:31

Watatu wauawa katika mripuko Mogadishu, Somalia

Watatu wauawa katika mripuko Mogadishu, Somalia

Kwa uchache watu watatu wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea mripuko wa bomu nje ya mkahawa mmoja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Shirika la habari la Reuters limemnukuu Abdul Fattah Omar, msemaji wa Baraza la Mji wa Mogadishu akisema leo mbele ya waandishi wa habari katika eneo ulipotokea mripuko huo kuwa, raia watatu wameuawa na wengine watano kujeruhiwa katika tukio hilo.

Hadi tunapokea habari hii, hakukuwa na kundi lolote lililotangaza kuhusika na mripuko huo.

Hata hivyo kidole cha lawama kinaelekezwa kwa kundi la kigaidi la ash Shabab, moja ya makundi ya mtandao wa al Qaida kutokana na kuwa na historia ya kufanya mashambulizi ya namna hiyo ndani na nje ya Somalia.

Shambulio hilo la kigaidi limetokea katika hali ambayo mwanzoni mwa mwezi huu wa Aprili makamanda saba wa kundi la ash Shabab waliuawa nchini Somalia katika oparesheni za pamoja za Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika AMISOM na jeshi la nchi hiyo.

Taarifa zilisema kuwa makamanda hao wa ngazi za juu wa ash Shabab waliuawa katika kipindi cha wiki moja ya tangu kuanza operesheni za askari wa AMISOM na Jeshi la Somalia.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …