Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 04 Septemba 2015 09:19

Nchi tatu kufanya kikao juu ya mgogoro wa Libya

Nchi tatu kufanya kikao juu ya mgogoro wa Libya

Nchi tatu za Chad, Niger na Algeria, zimepanga kufanya kikao maalumu kitakachojadili mgogoro wa Libya. Waziri wa Mambo ya Nje wa Algeria, Ramtane Lamamra amesema kuwa kikao hicho kitafanyika Algiers, mji mkuu wa Algeria. Amesema kuwa, katika kikao hicho ambacho kitaanza siku ya Jumapili ijayo, Waziri wa Masuala ya Kiafrika wa Algeria na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Niger na Chad, watajadili njia za namna ya kutatua mgogoro wa Libya kisiasa na chini ya uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo inaeleza kuwa, katika kikao hicho pia nchi tatu zitajadili pia masuala mbalimbali ya Algeria. Hii ni katika hali ambayo mazungumzo baina ya pande tofauti za mapigano nchini Libya, yalianza jana Alkhamisi huko Geneva, Uswisi chini ya uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa na yanatazamiwa kuendelea leo. Tayari mazungumzo hayo yameonyesha matarajio ya kufikiwa makubaliano katika kikao hicho. Libya imekuwa uwanja wa mapigano tangu ulipoondelewa madarakani utawala wa Kanali Muammar Gaddaf kupitia wimbi la mapinduzi ya wananchi lililoibuka mwaka 2011 huko kaskazini mwa Afrika.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …