Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 18 Machi 2012 18:53

Dua baada ya Sala ya Isha

بسم الله الرحمن الرحیم

اَللّهُمَّ اِنَّهُ لَيْسَ لي عِلْمٌ بِمَوْضِعِ رِزْقي وَاِنَّما اَطْلُبُهُ بِخَطَرات تَخْطُرُ عَلى قَلْبي فَاَجُولُ فى طَلَبِهِ الْبُلْدانَ فَاَنَا فيما اَنَا طالِبٌ كَالْحَيْرانِ لا اَدْري اَفى سَهْل هَوُ اَمْ في جَبَل اَمْ في اَرْض اَمْ في سَماء اَمْ في بَرٍّ اَمْ في بَحْر وَعَلى يَدَيْ مَنْ وَمِنْ قِبَلِ مَنْ وَقَدْ عَلِمْتُ اَنَّ عِلْمَهُ عِنْدَكَ وَاَسْبابَهُ بِيَدِكَ وَاَنْتَ الَّذي تَقْسِمُهُ بِلُطْفِكَ وَتُسَبِّبُهُ بِرَحْمَتِكَ اَللّهُمَّ فَصَلِّ عَلى مُحَمَّد وَآلِهِ وَاجْعَلْ يا رَبِّ رِزْقَكَ لي واسِعاً وَمَطْلَبَهُ سَهْلاً وَمَأخَذَهُ قَريباً وَلا تُعَنِّني بِطَلَبِ ما لَمْ تُقَدِّرْ لي فيهِ رِزْقاً فَاِنَّكَ غَنِىٌّ عَنْ عَذابي وَاَنَا فَقيرٌ اِلى رَحْمَتِكَ فَصَلِّ عَلى مُحَمَّد وَآلِهِ وَجُدْ عَلى عَبْدِكَ بِفَضْلِكَ اِنَّكَ ذُو فَضْل عَظيم

 

 

Bismillahir Rahmanir Rahim


Ewe Bwana wangu! Hakika yangu mimi siijui sehemu ilipo rizki yangu, bali ninaitafuta kwa kutegemea kila kinachonipitikia katika moyo wangu. Ninazunguka huku na huko kuitafuta katika miji, nikiendelea kutafuta bila ya kujua sehemu ilipo rizki yangu. Siju iko katika tambarare au katika jabali, au ardhini au mbinguni au nchi kavu au baharini. Na sijui iko mikononi mwa nani na inapitia kwa nani. Lakini nina yakini kwamba Wewe Ndiye unayejua ilipo rizki yangu na njia za kuipata ziko mikononi Mwako. Na ni Wewe Ndiye unayeitoa na kuitandaza kwa upole na rehema Zako. Bwana wangu! Mminie rehema Zako Muhammad na Aali Muhammad na ujaalie Ewe Bwana wangu, riziki yako kwangu iwe pana, na kuitafuta iwe rahisi na mahala pa kuipata pawe karibu na uniepushe kutafuta riziki sehemu ambapo haijakadiriwa kuwepo riziki yangu. Hakika Yako Wewe ni Mkwasi kuliko adhabu yangu na mimi ni fakiri ninayehitajia mno rehema Zako. Mmiminie rehema na amani Muhammad na Aali zake na nifanyie huruma mimi mja Wako kwa fadhila na rehema Zako. Hakika Yako Wewe una fadhila kubwa sana.

Zaidi katika kategoria hii: « Dua baada ya Sala ya Magharibi

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …