Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 09 Disemba 2010 16:53

Surat Yusuf - Aya ya 4-6

Sikiliza
Wasikilizaji wapenzi wa Darsa ya Qur'ani Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Bismillahir Rahmanir Rahim
Tunammshukuru Allah SWT ambaye ametupa taufiki ya kukutana tena katika mfululizo mwingine wa Darsa ya Qur'ani. Sura tunayoizungumzia kwa sasa ni ya 12 ya Yusuf ambapo katika darsa hii ya 35 tutaangazia yale yaliyomo kwenye aya ya 3 ya sura hiyo tukianza na aya ya 4 ambayo inasema:
Yusuf alipo mwambia baba yake:
Yusuf alipo mwambaia baba yake: Ewe babayangu! Hakika mimi nimeota nyota kumi na moja, na jua na mwezi. Nimeota zikinisujudia.
Kisa cha Nabii Yusuf AS ndani ya Quran kinaanza na ndoto iliyompa Nabii huyo mwanga wa matumaini mema juu ya mustakabali wake. Bwana Mtume SAW anasema ndoto ni namna tatu; namna ya kwanza ni ya bishara njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu , namna nyingine huwa ni juu huzuni na majonzi inatokana na shetani na namna ya tatu huhusu matatizo ya kila siku ya mtu ambayo huyaona usingizini ambayo huitafiri akili ya mtu'.
Tab'an ndoto wanazoota mawalii wa Mwenyezi Mungu huwa ni ndoto za kweli yaani huwa ni Wahyi wa Mwenyezi Mungu, kama ilivyotokea kwa Nabii Ibrahim kuona katika ndoto kuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu ni ndoto za kweli yaani huwa ni Wahyi wa Mwenyezi Mungu, kama ilivyotokea kwa Nabii Ibrahim kuona katika ndoto kuwa kwa amri ya Mwenyezi Mungu anamchinja mwanawe Ismail. Au pia ndoto hizo hubainisha hakika ya mambo yatakayojiri siku za usoni, kama ilivyokuwa katika ndoto ya Nabii Yusuf ambapo InshaAllah kama tutakavyokuja kuona mwishoni mwa kisa cha Mtume huyo, ni kwamba hatimaye alifikia kwenye cheo na daraja ya juu na ndugu zake 11 pamoja na baba na mama yake wakaporomoka kuonyesha taadhima mbele yake. Baadhi ya mafuno tunayopata kutokana na ayah ii ni kuwa ndoto ni mojawapo wa njia za kuelewa hakika na siri za mambo ambayo baadhi ya watu hawawezi kuyabaini. Funzo jengine tunalopata katika aya hii ni kuwa wazazi wanatakiwa wajenge mahusiano ya kushibana na watoto wao ili watoto wao waweze kujenga imani kamili kwao na kuwa tayari kuwaeleza masuala na yaleo yaliyomo moyoni mwao.
QASIDA
Tunaiendeleza darsa yetu kwa aya ya 5 ambayo inasema:
(Baba) akasema: Ewe mwanangu! Usiwasimulie nduguzo ndoto yako, wasije wakakufanyia vitimbi. Hakika Shet'ani ni adui dhaahiri kwa mwanaadamu.
Nabii Yaqub AS yaani baba wa Nabii Yusuf, alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Hivyo alibaini kwamba ndoto ya mwanawe haikuwa ya jambo la kawaida. Bali ilimaanisha utukufu na ukamilifu atakaoufikia katika mustakabali. Hivyo akamuusia aiweke siri hiyo kifuani mwaka na wala asije akawahadithiti ndugu zake, wakni si haska kaka zake hao wakaja wakamwonoea husda na hivyo kutaka kumdhuru. Kimsingi ni kwamba wazazi na watoto pia wanatakiwa wachunge na kulitahadahri suala la husuda baina ya watoto na hivyo wajihadharai kumsifu mmoja wa watoto wao kwa sifa au kipawa ikiwa ni cha kieleimu au pengeni uweledi wa kitu fulani, ili isije ikapelekea watoto wengine kujenga hisia mbaya dhidi ya mwenzao. Na ndiyo maana kama tuliyoona, Yusuf Mwenyewe aliamua kumsimulia baba yake ndoto yake bila kuwepo ndugu zake, na baba mtu akamtaka mwanawe alifanye jambo hilo kuwa siri ya moyoni mwaka. Miongoni mwa nukta za kuzingatiwa katika ayah ii ni kuwa kama ambavyo kusimulia mtu anayoyaona katika ndoto kunaweza kuzusha titian, haifai kusimulia pia kila tunaloliona tukiwa macho kwani si ajabu kufanya hivyo pia kukaweza kuwa sababu ya kuzuka fitina. Nukta nyingine ya kuzingatia katika ayah ii ni kwamba hatari ya husda ni kubwa, iwe ni katika mazingira ya ndani ya nyumba ua hata katika jamii; na moja ya njia muhimu ya kueppusha hatari yake ni mtu kubakisha kuwa siri ya moyoni mwake mambo yanayoweza kusababisha hali hiyo.
Aya ya 6 ya sura yetu ya Yusuf ndiyo inayotuhitimishia darsa yetu hii, aya hiyo inasema:
Na kadhaalika Mola wako Mlezi atakuteuwa na atakufundisha tafsiri ya mambo. Na atatimiza neema zake juu ukoo wa Yaqub, kama alivyo watimizia hapo zamani baba zake Ibrahim na Ishaq. Hakika Mola wako mlezi ni Mjuzi Mwenye Hekima.
Katika kuendelea kmuusia mwanawe, Nabii Yaaqub alimwaambai ewe Yusuf, katika mustakabali Mwenyezi Mungu atateua kuwa Mtume wake na kukamilisha neema zake kwa kizazi chetu ikiwa na pamoja na kukupa wewe ilmu ya kuagua ndoto itakayowezesha kubainisha hakika juu ya mambo mbali mbali. Kwa hakika utabiri huo wa Nabii Yaqub ulitokana na elimu ya ghaibu ambayo Allah SWT aliwatunuku Mitume wake na kuwafanya wajue yale yatakayuojiri siku za usoni. Mbali na kwamba Nabii Yaqub angeweza pia kutafsiri hivyo kutokana na dnoto aliyoota mwanawe yusuf. Baadhi ya mafunzo tunayopata kutokana na ayah ii ni kuwa Mwenyezi Mungu SWT huwachagua miongoni mwa waja wake walio bora kuwa mitume wake na kuwapa elimu inayohitajika kwa ajili ya kuwa waunganishi wa kifikisha uongofu wake kwa watu. Funzo jengine tunalopata kutokana na aya hjii ni kwamba dua iliyoombwa na Nabii Ibrahim AS ya kutaka Utume uendelee katika kizazi chake ilitakabaliwa na Allah SWT na hivyo kizazi chake kuptiwa wanawe wasili Ishaq na Ismail kilifika kwenye utume, na hii inabainisha kuendelea kuwepo waja wasafi na watakasifu ndani ya kizazi hicho kiteule. Kwa haya machache basi tunaifunga darsa yetu hii. Tunamuomba Allah SWT azitakase nyoto zetu na maradhi machafu ya husda, na kutuepusha na husda za wengine. Wasalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

 

Unaweza pia kusikiliza kwa kutumia: 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …