Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 21 Aprili 2008 21:47

Suratul Anfal: Aya ya 22-25

Assalamu Alaykum Warahamatullahi Wabarakaatuh. Bismillahi. Shukrani na sifa njema
zote zinamstahikia Allah sw, Muumba wa kila kitu. Tunaendelea na darsa ya yetu ya
quran inayotoa tarjumi na maelezo kwa ufupi ya kitabu kitukufu cha quran, kulingana na
mpangilio wa sura zake. Katika darsa hii tunaanza na aya ya 22 ya Sura yetu ya al-
Anfaal:


Hakika Vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni hawa wanaojipa uziwi (wa
kutosikia), wanaojipa ububu (wasiikiri hiyo haki), ambao hawayatii akilini
(wanayoambiwa, bali wanayakataa tu vivi hivi bila ya kuyapima kwanza).

Jambo linalomtafautisha mwanadamu na wanyama wengine ni akili na uwezo wake wa
kufikiria na kutafakari. Kwa msingi huo, watu wasiopima mambo kwa kutumia akili zao
au kuzungumza bila ya kutumia vipimo vya akili na mantiki, ni kama watu wasio na akili
na ni sawa kabisa na wanyama au kwa kauli ya Qur'ni yenyewe, wana hadhi ya chini
zaidi hata kuliko wanyama wa miguu mine. Hii ni kwa sababu, wanyama hawana akili
bali huendesha maisha yao kwa kutegemea ghariza na matamanio ilihali mwanadamu
mbali na kuwa na matamanio, lakini amepewa akili ambayo kwayo anapaswa
kupambanua mambo na kutofautisha kati ya mema na mabaya. Kwa hivyo, kama
hatatumia akili aliyopewa kwa lengo hilo atakuwa ni mbovu zaidi hata kuliko mnyama.
Aya hiyo inasema kuwa, thamani ya mwanadamu mbele ya Mwenyezi Mungu ni
kiwango cha akili yake, kusikiliza na kusema haki na kwamba mtu asiyeyazingatia hayo


huwa hana thamani yoyote mbele ya Muumba wake, bali thamani yake huwa ni ya chini
kabisa hata kuliko ya mnyama.
Kwa mujibu wa aya ya 10 ya Surat al-Mulk pia, watu wa Motoni watataja sababu ya
kuwa kwao motoni kwa kusema:

 

"Kama tungalikuwa tunasikia au tungalikuwa na akili hatungekuwa katika watu wa
Motoni (leo)."

Tunajifunza mambo kadhaa kutokana na aya hii:
1-Masikio, macho na ulimi huwa na thamani kwa mwanadamu kama atavitumia
viungo hivyo muhimu katika njia ya kudiriki na kuikubali haki.

2-Thamani ya mwanadamu inafungamana na uzingatiaji wake wa akili na busara na
kwamba, kujiweka kwake mbali na mafundisho ya Mwenyezi Mungu hakuoani
hata kidogo na akili.

Ifuatayo sasa ni aya ya 23 ambayo inasema:


Na kama Mwenyezi Mungu angalijua wema wowote kwao, angewasikilizisha; na kama
angeliwasikilizisha wangeligeuka (vilevile) wakapuuza.


Aya hii inazungumzia watu ambao walikuwa na masikio lakini wakijifanya viziwi mbele
ya maneno ya haki, na waliokuwa na ndimi lakini wakijifanya mabubu na kutotaka kukiri
ukweli. Aya hiyo inasema kwamba, hata kama Mwenyezi Mungu alikuwa na uwezo wa
kupenyeza haki katika nyoyo zao lakini matendo yao maovu yalikuwa ni makubwa kiasi
kwamba, yalikuwa yameondoa kabisa mazingira ya kuwawezesha wao kukubali na kukiri
haki. Hakukuwepo tena na wema wala kheri katika nyoyo hizo. Mbali na hayo, walikuwa
wamezama kwenye ukaidi na inadi kiasi kwamba, hata kama wangeona wazi ukweli na
haki katika aya za Mwenyezi Mungu, lakini wasingekuwa tayari kukubali haki hiyo.
Tunajifunza yafuatayo kutokana na aya hii:
Ada na sunna ya Mwenyezi Mungu ni kuwa, humpa taufiki mja ambaye huwa
amejitayarisha na kujiandalia mazingira ya kupata taufiki hiyo.
Ada na kanuni za Mwenyezi Mungu zimejengeka katika msingi kwamba, mwanadamu
amepewa hiari ya kujiamulia mambo yake mwenyewe. Pamoja na kuwa Mwenyezi
Mungu ana uwezo wa kumlazimisha aikubali haki, lakini wakati huohuo amempa hiari ya
kuikataa haki hiyo.
Sasa tunaendelea na aya ya 24 ya Sura hii:


Enyi Mloiamini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume wake anapokuiteni katika yale
yatakayokupeni uhai mzuri (wa dunia na Akhera. Fuateni amri zake Mwenyezi Mungu na
makatazo yake). Na jueni ya kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake(mara akafa. Basi asiakhirisheakhirishe kwa kutumaini uhai; na jueni). Kuwa kwake
Yeye mtakusanywa (mulipwe kwa kila mlilolifanya).

Aya hii inamsihi mwanadamu kuishi humu duniani maisha yaliyo juu ya kiwango cha
maisha ya mnyama. Maisha ambayo yatampelekea kustawi kiakili na kimaanawi, na njia
pekee ya kufikia maisha kama hayo ni kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu pamoja na
kutii amri za Mitume wake kama inavyosema aya ya 97 ya Surat an-Nahl:


Wafanyaji mema, wanaume au wanawake hali ya kuwa ni Waislamu, tutawahuisha
maisha mema, na tutawapa ujira wao (Akhera) mkubwa kabisa kwa sababu ya yale
mema waliyokuwa wakiyatenda.

Tunasoma katika aya za 29 na 30 ya Surat Aali Imran kama ifuatavyo:


Sema: Kama mkificha yaliyomo vifuani mwenu au mkiyadhihirisha (Mungu atakulipeni
tu kwani) Mwenyezi Mungu anayajua; na anayajua yaliyomo mbinguni na yaliyomoardhini; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza juu ya kila kitu. Siku ambayo kila nasfi
itakuta mema iliyoyafanya yamehudhurishwa, na pia ubaya ilioufanya. Itapenda lau
kungekuwa na masafa marefu baina ya ubaya huo na yeye. Na Mwenyezi Mungu
anakutahadharisheni na adhabu yake. Na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja (wake).

Anasema katika aya nyingine ya 16 ya Surat al-Qaf:


Nasi tu karibu naye zaidi kuliko mshipa wa shingo (yake).

Tunajifunza yafuatayo kutokana na aya inayojadiliwa:
1-Maisha mazuri na halisi ya mwanadamu yanapatikana katika mafundisho ya
Mitume, na bila ya mafundisho hayo, mwanadamu huwa ni maiti hata kama
ataonekana kunywa maji na kula chakula.

2-Kabla ya Mwenyezi Mungu kuwa uzio kati yetu na nyoyo zetu na mauti kutupata,
tunapasa kukubali haki na kufikiria juu ya maisha yetu ya milele huko Akhera.
Aya ya 25 inasema:


Na iogopeni adhabu (ya Mwenyezi Mungu ya hapa duniani) ambayo haitawasibu peke
yao wale waliodhulumu nafsi zao miongoni mwenu (bali itawasibu hata walionyamazawasiwakataze, bali na wengineo pia); na jueni ya kuwa Mwenyezi Mungu ni mkali wa
kuadhibu.

Baadhi ya wakati dhambi hufanyika kwa siri na kwa namna ambayo huwa ni mtu binafsi
ndiye huhusika nayo moja kwa moja na madhara pamoja na adhabu yake kumpata yeye
tu bila ya kuwakumba watu wengine. Lakini mara nyingine dhambi na maovu hufanyika
hadharani kadiri kwamba, huenea na kuwaathiri watu wengine katika jamii. Huenda
baadhi ya watu wakavutiwa na maovu hayo na hatimaye kuyachukulia kuwa jambo la
kawaida na lisilo na tatizo lolote la kisheria. Aya hii inasema kuwa, kama dhambi na
maovu yataachwa yaenee katika jamii na walio na uwezo wa kuyazuia kukaa kimya
wasichukue hatua yoyote ya kuyazuia, adhabu ya Mwenyezi Mungu huwapata wote
walio katika jamii hiyo. Kwa hivyo, madhumuni ya kuogopa adhabu ambayo haitawasibu
peke yao wale waliodhulumu nafsi zao miongoni mwao, sio kujitenga na jamii, bali ni
kuwa mwangalifu na kuchukua tahadhari dhidi ya maovu yanayotendeka kwenye jamii.
Kutokana na aya hii tunajifunza yafuatayo:

1-Kujiweka mbali mwanadamu na mafundisho ya Mwenyezi Mungu huleta fitina na
ufisadi katika jamii.
2-Hatupasi kuwa wafitini, kuwaunga mkono wafitini wala kunyamaza kimya mbele
ya fitina.

3-Kukataza mabaya ni jukumu la kila mtu muumini ambapo kama hakutakuwa na
athari yoyote katika kuzuia maovu basi bila shaka kutakuwa na athari katika
kuzuia kuteremka kwa adhabu ya Mwenyezi Mungu.

Wassalamu.../

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)

Hadithi ya Uongofu (39)

Ni matarajio yangu kuwa, hamjambo wapenzi wasikilizaji na tunakutana tena katika sehemu nyingine ya kipindi hiki cha Hadithi ya Uongofu. …

Ufeministi, Itikadi na Misingi yake (26)

Assalaamu Alaykum wafuatiliaji wa kipindi hiki na karibuni kuwa nasi katika sehemu nyingine ya kipindi hiki kinachokosoa itikadi ya ufeministi …

Ulaji wa Lishe Bora katika Kipindi Chote cha Maisha

Wataalamu wa Afya wanasema kuwa, awamu mbalimbali za maisha zinahitajia ulaji wa chakula wa aina tofauti. Iwapo wewe ni mtoto, …

Maua mawili ya Mtume wa Allah (31) Sauti

Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh Karibuni wapenzi wasikilizaji wa Idhaa ya Kiswahili Radio Tehran na wasomaji wa mtandao …