Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 03 Januari 2016 11:38

Barua ya Kiongozi Muadhamu ina thamani kubwa

Barua ya Kiongozi Muadhamu ina thamani kubwa

Mwandishi na mtafiti wa Sayansi ya Kiislamu wa nchini Italia amesema kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi ina thamani kubwa sana na ni yenye taathira.

Carlo Crobucci mwanasheria, mwandishi na mtafiti wa Sayansi ya Kiislamu wa nchini Italia amebainisha kuwa, barua ya Ayatullah Ali Khamenei kwa vijana wa Magharibi ina umuhimu mkubwa ingawa inasikitisha kuwa, katika jamii ya Magharibi habari zinazohusiana na barua hiyo hazijaakisiwa kikamilifu na kwa njia sahihi.

Msomi huyo wa Kiitalia amesisitiza kuwa, katika ulimwengu wa Magharibi habari zote zinazohusiana na jinai za kweli zinazotokana na uroshaji mabomu, vita na umwagaji damu pamoja na uvamizi wa madola ya Magharibi katika maeneo mbalimbali duniani zimekuwa zikifichwa na kutoakisiwa. Aidha Carlo Corbucci amesifu hatua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya kuwaandikia barua vijana wa Magharibi na kuwaamsha kuhusiana na mambo mbalimbali yanayojiri katika jamii zao.

Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)