Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 28 Disemba 2015 11:32

Barua ya Kiongozi, tahadhari kwa vijana dhidi ya unafiki wa Magharibi

Barua ya Kiongozi, tahadhari kwa vijana dhidi ya unafiki wa Magharibi
Mark Dankof, mtaalamu wa masuala ya kisiasa nchini Marekani amesema barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi inalenga kuwaamsha na kuwatahadharisha vijana sio tu wa Magharibi bali katika maeneo yote duniani dhidi ya unafiki na sera za undumakuwili za nchi za Magharibi kwa nchi nyinginezo.

Dankof ambaye pia aliwahi kuwania useneta nchini Marekani amesema barua hiyo ina umuhimu mkubwa sana kwa tabaka la vijana na kuongeza kuwa risala hiyo ni moja ya jumbe mbili nyeti alizozisoma mwaka huu wa 2015, ya pili ikiwa ni kitabu kilichopewa anwani isemayo "Mwisho wa Ukomunisti, ni mwisho wa demokrasia Magharibi" ambacho toleo la kwanza lilichapishwa mwaka 1999 na mwanaharakati Alexander Zinoviev.

Mchambuzi huyo wa masuala ya siasa wa Marekani amesema barua hiyo imekuja wakati mwafaka na kwamba kila Mmarekani ima ni mfuasi wa chama cha Republican au Democrat anafaa kuisoma ili kufahamu chimbuko la ugaidi haswa katika kipindi hiki nyeti cha kampeni za urais ambapo baadhi ya wanasiasa wanajitafutia umaarufu kwa kueneza chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Msomo huyo amesema barua ya Kiongozi Muadhamu imeweka wazi ukweli mchungu ambao vijana wengi wa Magharibi hawaujui, kuwa kuna zaidi ya Waislamu bilioni 1.5 duniani na kwamba waumini wa dini hiyo tukufu ndio wahanga wakuu wa ugaidi licha ya wao kuelekezewa kidole cha lawama kila kunapotokea shambulizi la ugaidi.

Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)