Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 25 Disemba 2015 19:23

“Barua ya Kiongozi, mwanga wa kujua Uislamu”

“Barua ya Kiongozi, mwanga wa kujua Uislamu”

Mchanganuzi mmoja wa masuala ya siasa nchini Marekani amesema barua iliyoandikwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi inalenga kulizindua na kulifahamisha tabaka la vijana ukweli kuhusu Uislamu wa Waislamu.

Keith Preston ambaye pia ni mhariri na mkurugenzi wa mtandao wa ‘attackthesystem.com’ amesema barua hiyo ya Kiongozi Muadhamu Ayatullah Ali Khamenei inafafanua misingi na mafundisho sahihi ya Uislamu sambamba na kuondoa kasumba na propaganda ambazo zimekuwa zikitumiwa na Wamagharibi hususan Wamarekani kupotosha watu kuhusu Uislamu. Amesema barua hiyo inaweka wazi historia, mila na utamaduni wa Uislamu na Waislamu pamoja na kuondoa taka za masikioni kuhusu ulimwengu wa Kiislamu.

Ikumbukwe kuwa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliwaandika barua vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi duniani hasa ya mashambulizi ya Ufaransa Novemba 13 ambapo makumi ya watu waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)