Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 24 Disemba 2015 18:21

Qanaat: Barua ya Kiongozi Muadhamu inaeleza umuhimu wa kuujua ugaidi

Qanaat: Barua ya Kiongozi Muadhamu inaeleza umuhimu wa kuujua ugaidi
Mkuu wa Jumuiya ya Wasomi wa Madhehebu ya Ahlul Bayt mjini Istanbul, Uturuki amesema kuwa, barua ya pili ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi inabainisha umuhimu wa kutambua na kuuelewa vyema ugaidi.

Hassan Qanaat amebainisha kwamba, barua hiyo ya Ayatullah Ali Khamenei inautambulisha na kuuleza ugaidi kuwa ni maumivu ya pamoja ya wanadamu wote na kwamba, sio jambo linalowahusu watu fulani.

Mwanaharakati huyo wa Kiislamu amesema kuwa, katika barua hiyo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi amebainisha na kuweka wazi mambo ya leo yanayoikabili jamii ya mwanadamu na ulazima wa fikra za waliowengi kuweka wazi mambo haya mkabala na shubha na njama za maadui. Ameongeza kuwa, katika barua hiyo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewataka vijana kujiandaa kukabiliana na fitina za aina mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)