Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 24 Disemba 2015 06:09

"Barua ya Kiongozi Muadhamu ina ujumbe wa kibinadamu"

 "Barua ya Kiongozi Muadhamu ina ujumbe wa kibinadamu"

Katibu Mkuu wa Mkutano wa Maaskofu Uswisi amesema kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi ina ujumbe wa kibinadamu.

Dr. Tadej Strehovec, amesema kuwa, barua hiyo haitambui Uislamu wala Ukristo bali imebeba ujumbe wa kibinadamu. Katibu Mkuu wa Mkutano wa Maaskofu Uswisi amesema kama ninavyomnukuu: " Nimeisoma barua ya Kiongozi Muadhamu na jambo ambalo limenishangaza ni kuwa, hakuna gazeti lolote miongoni mwa magazeti yetu ambalo limeizungumzia barua hii." Amesema kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amediriki suala hili kwamba, ukweli umejificha nyuma ya mashambulio ya kigaidi na jambo hili linaongeza umuhimu wa kuweko mazungumzo baina ya dini mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)