Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 22 Disemba 2015 11:18

'Barua ya Kiongozi imejaa ukweli wa kimaanawi'

'Barua ya Kiongozi imejaa ukweli wa kimaanawi'

Mhadhiri mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Lethbridge nchini Canada amesema barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi imejaa ukweli wa kimaanawi ambao unahusu watu wa rika na zama zote.

Profesa Anthony James Hall, ambaye ni mhadhiri wa masomo ya utandawazi nchini Canada amesema mbali na kuwa barua hiyo inawahusu watu wa matabaka yote, lakini zaidi inayahusu makabila, dini, mataifa na idiolojia zote. Msomi huyo amesema ugaidi ni zimwi katika karne hii na kwamba kuna haja kwa vijana wa kizazi hiki na vizazi vijavyo wafahamishwe ukweli kuhusu chimbuko la jinamizi hilo linalosambaa kwa kasi kubwa katika kila pembe ya dunia. Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)