Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 22 Disemba 2015 05:06

"Barua ya Kiongozi ina ujumbe wa matumaini"

"Barua ya Kiongozi ina ujumbe wa matumaini"

Mtaalamu mmoja wa masuala ya kisiasa wa nchini Afghanistan amesema kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwa vijana wa Magharibi ilikuwa na ujumbe wa matumaini na umaanawi.

Abdul-Shakuur Akhlaqi amesema kuwa, kwa kuzingatia kwamba, jamii wa Magharibi imepiga hatua katika uga wa teknolojia lakini iko dhaifu mno katika upande wa utu na umaanawi na inatangatanga katika suala la utambulisho wa kimaanawi, barua hiyo ya Kiongozi Muadhamu inaweza kuleta matumaini na kuwa na nafasi muhimu katika suala la umaanawi.

Abdul-Shakuur Akhlaqi ameongeza kuwa, katika barua hiyo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha kwamba, ubinadamu haupatikani tu katika ustawi wa kimaada na maendeleo ya teknolojia, bali mwanadamu wa kweli anahitajia umaanawi na huba.

Mtaalamu huyo wa masuala ya kisiasa wa nchini Afghanistan ameashiria undumakuwili wa Magharibi katika suala la ugaidi na kusema kuwa, kwa miaka mingi sasa wananchi wa Afghanistan wamekuwa wakipambana na ugaidi.

Amesema kuwa, uwepo wa vikosi vya kigeni nchini Afghanistan kwa kisingizio cha kudhamini usalama, sio tu kwamba, haujapelekea kupungua ukosefu wa usalama bali ukosefu wa amani na usalama umezidi kuongezeka katika nchi hiyo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)