Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 20 Disemba 2015 18:28

'Barua ya Kiongozi Muadhamu ina umuhimu mkubwa'

'Barua ya Kiongozi Muadhamu ina umuhimu mkubwa'
Mtaalamu mmoja wa masuala ya kimataifa wa nchini Mexico amesema kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa nchi za Magharibi ina umuhimu mkubwa.

Acosta Rivero, mtaalamu wa masuala ya kimataifa wa nchini Mexico amesema leo kwenye mahojiano na Idhaa ya Kihispania ya Radio Tehran kwamba, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi ina umuhimu mkubwa na inabidi wananchi wote wa Marekani, Ulaya na kote ulimwenguni wazingatie mafundisho sahihi na halisi ya dini tukufu ya Kiislamu.

Aidha amesema, barua hiyo ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu inaweza kutoa msukumo mkubwa kwa Waislamu kujituma na kushiriki vilivyo katika kutangaza na kueneza mafundisho ya Uislamu wa kweli kupitia maneno na vitendo vyao.

Vile vile amemnukuu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akisema kupitia barua hiyo kwamba, watu waliofanya operesheni za kigaidi mjini Paris Ufaransa ni wale wale waliofanya mashambulizi kama hayo dhidi ya Waislamu mjini Beirut Lebanon, siku chache kabla ya mashambulio hayo ya Paris.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)