Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 20 Disemba 2015 07:12

Barua ya Kiongozi Muadhamu ina nafasi muhimu katika kubadilisha mtazamo wa vijana wa Magharibi kuhusu Uislamu

Barua ya Kiongozi Muadhamu ina nafasi muhimu katika kubadilisha mtazamo wa vijana wa Magharibi kuhusu Uislamu
Ali Iqbal, mtaalamu wa masuala ya kisiasa wa nchini Afghanistan amesema kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi ina nafasi muhimu sana katika kubadilisha mtazamo wa vijana hao kuhusiana na Uislamu.

Mchambuzi huyo wa masuala ya kisiasa amesema kuwa, kwa kuzingatia siasa za nchi za Magharibi za kueneza wimbi la chuki dhidi ya Uislamu katika ulimwengu wa Magharibi na kutoa himaya ya kifedha na kisilaha kwa makundi yenye misimamo mikali lengo likiwa ni kuchafua sura halisi ya Uislamu, barua ya Ayatullah Ali Khamenei kwa vijana wa Magharibi katika mazingira haya inaweza kuwa na nafasi muhimu mno katika kubadilisha mtazamo wa vijana hao kuhusiana na Uislamu na kuondoa taswira mbaya waliyonayo kuhusiana na dini hii tukufu.

Ali Iqbal, ameashiria siasa za kindumakuwili za Magharibi katika kukabiliana na ugaidi nukta ambayo imeashiriwa pia na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu katika barua yake hiyo na kusema kuwa, madola ya Magharibi yanasema uongo kwa kudai kwamba, yanapambana na ugaidi ilihali yanayaunga mkono makundi ya kigaidi na hata kuyapatia misaada ya silaha na fedha.

Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)