Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 19 Disemba 2015 22:07

Barua ya Kiongozi Muadhamu kwa vijana wa Magharibi ni yenye kuwaamsha

Barua ya Kiongozi Muadhamu kwa vijana wa Magharibi ni yenye kuwaamsha

Mwandishi wa habari wa Afghanistan amesema kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi ina ujumbe wenye kuwaamsha vijana hao.

Vahid Mozhdehamesema kuwa, katika mazingira ambayo Wamagharibi wanafanya njama za kuutwisha Uislamu na Waislamu matatizo na changamoto zote, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akaona kuna udharura wa kuandika barua kama hii ambayo inawaamsha vijana wa Magharibi.

Mwandishi huyo wa habari amebainisha kuwa, propaganda chafu za kuuogopesha Uislamu zimekuwa zikifanywa katika ulimwengu wa Magharibi na waungaji mkono wa utawala haramu wa israel lengo likiwa ni kuitia dosari dini tukufu ya Kiislamu.

Amesema, Uislamu umehatarisha maslahi ya ukoloni wa magharibi na ndio maana viongozi wa nchi hizo wamekuwa nyuma ya proganda hizo.

Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita. Barua hiyo ambayo ni ya pili kwa vijana wa Magharibi baada ya ile ya Januari imeendelea kuakisiwa kote duniani huku wasomi na vijana wanaharakati wakisema imekuja wakati unaofaa kwani kunaenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi pasina vijana wa nchi hizo kujua ukweli kuhusu Uislamu na Waislamu. Mapema Januari mwaka huu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alituma barua nyingine kwa vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini ambapo aliwataka vijana kufanya uchunguzi na udadisi kuhusu misukumo na malengo ya kufanyika kampeni kubwa mno ya kuenezwa sura isiyo sahihi kuhusiana na Uislamu.

 

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)