Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumanne, 15 Disemba 2015 06:52

Barua ya Kiongozi kwa vijana ni ya kimantiki

Barua ya Kiongozi kwa vijana ni ya kimantiki

Barua ya pili ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana Wamagharibi ni ya kimantiki, amesema Daniel Tout mchambuzi wa masuala ya kisiasa kutoka Slovakia.

Katika mahojiano na Radio Tehran, ameongeza kuwa barua hiyo pia ni ishara ya hadhi ya juu aliyonayo Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu. Mchamabuzi huyo wa Slovakia amebainisha masikitiko yake kuwa vijana wa nchi za Magharibi wanakabiliwa na hujuma za habari za upotoshaji kutoka katika vyombo vya habari vya nchi za Magharibi. Ameendelea kusema kuwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameonyesha kuwa Uislamu halisi ni dini yenye mapenzi.

Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita. Barua hiyo ambayo ni ya pili kwa vijana wa Magharibi baada ya ile ya Januari imeendelea kuakisiwa kote duniani huku wasomi na vijana wanaharakati wakisema imekuja wakati unaofaa kwani kunaenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi pasina vijana wa nchi hizo kujua ukweli kuhusu Uislamu na Waislamu. Mapema Januari mwaka huu Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu alituma barua nyingine kwa vijana wa Ulaya na Amerika Kaskazini ambapo aliwataka vijana kufanya uchunguzi na udadisi kuhusu misukumo na malengo ya kufanyika kampeni kubwa mno ya kuenezwa sura isiyo sahihi kuhusiana na Uislamu.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)