Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 14 Disemba 2015 19:14

"Barua ya Kiongozi Muadhamu ina umuhimu mkubwa"

 "Barua ya Kiongozi Muadhamu ina umuhimu mkubwa"

Mwanachama wa Tume ya Haki za Binadamu ya Kiislamu (IHRC) yenye makao yake mjini London, Uingereza amesema kuwa barua iliyoandikwa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei kwa vijana wa Magharibi inaakisi muono wa mbali na mtazamo sahihi wa kiongozi huyo.

Nazem Ali ambaye ni mwanachama wa IHRC ameiambia IRIB kwamba, hatua ya Kiongozi Muadhamu ya kuwaandikia barua vijana wa nchi za Magharibi akiwataka kutambua vyema Uislamu na kwamba wasiviamini vyombo vya habari vinavyoeneza propaganda za uongo ina umuhimu mkubwa na mtazamo mpana.

Nazem Ali ameongeza kuwa, suala hilo pia linaonesha njia ya kidemokrasia kwa ajili ya kuchagua kwa uhuru mtazamo wowote kuhusu masuala ya kimataifa. Amesema Ayatullah Khamenei amewataka vijana wa Magharibi wajitenge na mitazamo ya kutwishwa na kulazimishwa na watafakari kwa uhuru kuhusu masuala mbalimbali.

Mtaalamu huyo wa masuala ya kisiasa anasema kuwa, nchi za Magharibi zinatumia makundi ya kigaidi kuvuruga usalama na amani ya nchi nyingine na kuchochea vita na machafuko katika nchi hizo. Ameongeza kuwa Magharibi pia inafanya njama za kuchafua sura ya Uislamu katika fikra za walimwengu kwa kuanzisha na kufadhili makundi kama Al Qaida, Jabhatu Nusra na Daesh.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)