Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 14 Disemba 2015 04:49

Njama ya Riyadh ya kutoenezwa barua ya Kiongozi

Njama ya Riyadh ya kutoenezwa barua ya Kiongozi

Huku barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi ikiendelea kuakisiwa kwa wingi na vyombo vya habari duniani, utawala wa Saudi Arabia unafanya juu chini kuhakikisha kuwa barua hiyo haisomwi na kuenezwa kwenye mitandao ya kijamii nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya kanali ya televisheni ya al-Manar ya Lebanon, utawala wa aal-Saud unayashinikiza mashirika ya Google, Twitter na Facebook kuzuia kusambazwa kwa barua hiyo katika mitandao ya kijamii, ambayo hutumiwa aghalabu na tabaka la vijana. Mwanamfalme Alwaheed bin Talal bin Abdulaziz Aal Saud ambaye ni mmoja wa shakhsia wenye hisa kubwa zaidi kwenye shirika la Twitter, ametoa wito wa kuzuiwa kuenezwa kwa barua hiyo katika mitandao mingine mashuhuri ya kijamii pasina kutoa sababu zozote za msingi. Hii ni katika hali ambayo, wataalamu wa masuala ya kisiasa na wachanganuzi wa mambo wanaendelea kuipongeza barua hiyo, wakisema kuwa, imekuja wakati mwafaka na kubatilisha njama za Magharibi za kueneza chuki dhidi ya Uislamu. Aidha wasomi na wanafikra wanasema harakati za baadhi ya vyombo vya habari vya Kiislamu ni dhaifu katika kuutangaza Uislamu kwa njia sahihi katika jamii za Magharibi na kusisitiza kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu itatoa mchango mkubwa katika kuutangaza vizuri zaidi Uislamu wa kweli kwenye nchi hizo.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)