Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumapili, 13 Disemba 2015 18:31

Vatican yapongeza barua ya Kiongozi kwa vijana

Vatican yapongeza barua ya Kiongozi kwa vijana

Afisa mwandamizi wa makao makuu ya Kanisa Katoliki duniani Vatican ameitaja barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi kuwa ni muhimu na yenye taathira.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la IRIB, Kadinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Mkuu wa Kamati ya Papa ya Uadilifu na Amani amesisitiza kuwa, barua ya Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imekuwa na taathira katika kutayarisha mazingira bora ya mazungumzo baina ya mataifa. Ameongeza kuwa, katika barua hiyo, Kiongozi Muadhamu amewataka vijana Wamagharibi waangazie upya matukio ya kihistoria na yale yanayojiri katika dunia ya leo. Amewataka vijana wawe huru katika mitazamo yao na waangalie mambo kwa mtazamo mpya."

Kadinali Turkson amesema moja kati ya mihimili mikuu ya barua ya pili ya Kiongozi Muadhamu kwa vijana wa Magharibi ambayo ameipokea rasmi kutoka kwa balozi wa Iran Vatican, imelenga pia kukabiliana na chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi. Kadinali huyo ameongeza kuwa, haipaswi kulinganisha Uislamu au dini nyingine yoyote na utumiaji mabavu kwani ujumbe wa dini zote za Tauhidi ni ujumbe wa Mwenyezi Mungu wa amani na hivyo ukatili wa aina yoyote unapaswa kunasibishwa na watu binafsi na wala si dini.

 

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)