Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 12 Disemba 2015 18:04

Barua ya Kiongozi Muadhamu yaakisiwa kwa wingi duniani

Barua ya Kiongozi Muadhamu yaakisiwa kwa wingi duniani

Mtaalamu mmoja wa masuala ya kisiasa amesema kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi imeakisiwa kwa wingi na vyombo vya habari duniani.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiarabu ya Radio Tehran, Bw Ahmad al Bahrani amegusia mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni ya mjini Paris Ufaransa na kusema kuwa, barua hiyo ya Kiongozi Muadhamu imekuja wakati mwafaka na kubatilisha njama za Magharibi za kueneza chuki dhidi ya Uislamu.

Mtaalamu huyo wa masuala ya kisiasa na ya ulimwengu wa Kiislamu ameongeza kuwa, barua iliyojaa hekima na busara ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu imepokewa vizuri na wasomi na watu wenye ushawishi katika nchi za Magharibi.

Vile vile amesema, harakati za baadhi ya vyombo vya habari vya Kiislamu ni dhaifu katika kuutangaza Uislamu kwa njia sahihi katika jamii za Magharibi na kusisitiza kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu itatoa mchango mkubwa katika kuutangaza vizuri zaidi Uislamu wa kweli kwenye nchi za Magharibi.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)