Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumamosi, 12 Disemba 2015 11:28

Waafghani wapongeza barua ya Kiongozi Muadhamu

Waafghani wapongeza barua ya Kiongozi Muadhamu

Vijana na wanachuo wa jimbo la Badakhshan nchini Afghanistan wameipokea kwa mikono miwili barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa nchi za Magharibi.

Vijana na wanachuo hao wamesema kuwa, barua hiyo ina nafasi muhimu katika kutambua ukweli na matukio yanayojiri leo katika maeneo mbalimbali ulimwenguni. Wanachuo na vijana hao wamesema kuwa, kwa kuzingatia kwamba, vijana ni taifa la kesho, barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ni ufumbuzi na mfungua njia katika uwanja huo. Wamesema kuwa, vijana wanapaswa kutambua mambo mabaya na mazuri ili waweze kujenga nchi zao.

Qudratullah mmoja wa wananchuo hao amesema kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel ni mfano wa wazi wa ugaidi wa kiserikali na kwamba, Wazayuni kwa zaidi ya miaka 60 sasa, wamekuwa wakiuwa na kutekeleza vitendo vya kinyama dhidi ya Wapalestina.

Ikumbukwe kuwa, Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliwaandika barua vijana wa Magharibi na kusema kuwa, alipata msukumo wa kuandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya mjini Paris, Ufaransa ya tarehe 13 mwezi uliopita.

Barua hiyo ambayo ni ya pili ya Ayatullah Ali Khameni kwa vijana wa Magharibi baada ya ile ya mwezi Januari, imeendelea kuakisiwa kote duniani huku wasomi, vijana na wanaharakati wakisema imekuja wakati unaofaa kwani hivi sasa kumeenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi pasi na vijana wa nchi hizo kujua ukweli kuhusu Uislamu na Waislamu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)