Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 11 Disemba 2015 11:32

"Barua ya Kiongozi ina himizo la Maadili ya Kiislamu"

"Barua ya Kiongozi ina himizo la Maadili ya Kiislamu"

Mwakilishi wa Faqihi Mtawala Katika Jumuiya ya Hilali Nyekundu ya Iran amesema barua ya hivi karibuni ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa nchi za Magharibi ni hatua katika kuhimiza na kueneza maadili ya Kiislamu.

Hujjatul Islam wal Muslimin Abdul Hussein Moez, ameongeza kuwa, jamii inahitajia maadili ya Mtume wa Uislamu SAW na huruma za Kiislamu. Amesema barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi imetumwa kwa msingi wa kuhimiza maadili ya Kiislamu na Sira ya Mtume Mtukufu SAW. Hujjatul Islam wal Muslimin Abdu Hussein Moez amebainisha kuwa Uislamu unazidi kustawi na kuenea Ulaya na kwamba maadui wanaeneza chuki dhidi ya Uislamu ili kujaribu kukabiliana na mkondo huo. Mwanazuoni huyo ameongeza kuwa, barua ya Kiongozi Muadhamu kwa vijana wa Magharibi imetolewa katika hali ambayo maadui wanatumia kundi la kigaidi la Daesh au ISIS kuchafua jina la Uislamu.

Ikumbukwe kuwa Ayatullah Khamenei Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliandika barua kwa vijana wa Magharibi na akasema aliandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya Ufaransa tarehe 13 mwezi uliopita. Barua hiyo ambayo ni ya pili kwa vijana wa Magharibi baada ya ile ya Januari imeendelea kuakisiwa kote duniani huku wasomi na vijana wanaharakati wakisema imekuja wakati unaofaa kwani kunaenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi pasina vijana wa nchi hizo kujua ukweli kuhusu Uislamu na Waislamu

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)