Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Ijumaa, 11 Disemba 2015 06:59

"Barua ya Kiongozi ni wenzo wa utatuzi wa matatizo"

"Barua ya Kiongozi ni wenzo wa utatuzi wa matatizo"

Mhadhiri mmoja wa Chuo Kikuu wa Kipalestina amesema barua ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi ni njia ya utatuzi wa matatizo yanayotokana na siasa za madola ya Magharibi duniani.

Dakta Abdulaqis ambaye ni mhadhiri wa taaluma ya Sayansi ya Siasa ameashiria kuzidi kuakisiwa na kufuatiliwa barua ya pili ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei kwa vijana wa Magharibi na kueleza kwamba, kwa kuzingatia matatizo yaliyoutanza ulimwengu kutokana na siasa za madola ya Magharibi, katika barua ya Ayatullah Khamenei zimebainishwa njia za ufumbuzi zenye faida kwa ajili ya kuyavuka matatizo hayo. Msomi na mtaalamu huyo wa Kipalestina ameashiria pia njama za ukufurishaji wa Kiwahabi na Wazayuni za kutaka kuutangaza Uislamu kuwa ni dini ya mauaji, ukatili na utekaji nyara watu na kufafanua kuwa, katika barua yake, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewatupia masuali kadhaa vijana wa Magharibi ya kuwataka wafanye utafiti ili kuja ukweli na sura halisi ya Uislamu ambayo ni dini ya huruma na usamehevu.

Dakta Abdulaqis amegusia pia nafasi ya barua ya Kiongozi Muadhamu katika duru za kimataifa na kutarjumiwa barua hiyo kwa lugha nyenginezo na kuongeza kuwa, bila ya kutaka kuonyesha kuwa mtazamo wake ni ukweli mutlaki na kuwalazimisha vijana wa Magharibi waufuate, Kiongozi Maudhamu amezitupia duru za Magharibi masuali ya kuzitaka zifanye utafiti ili kuweza kufikia kwenye hakika na ukweli wa mambo.../

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)