Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Alkhamisi, 10 Disemba 2015 11:14

"Barua ya Kiongozi, fursa ya mazungumzo duniani"

"Barua ya Kiongozi, fursa ya mazungumzo duniani"

Mchanganuzi mmoja mashuhuri wa nchini Lebanon ameipongeza barua ya pili ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa vijana wa Magharibi na kusema kuwa, risala hiyo inatoa fursa kwa ulimwengu wa Kiislamu kufanya mazungumzo na kujadiliana kuhusu changamoto zinazowakabili.

Amin Hoteit, ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya kijeshi na kiistratejia amesema, barua hiyo imeandaa mazingira ya Waislamu kujadiliana kuhusu malengo yao ya thamani kama vile suala la usalama katika nchi za Kiislamu.

Mwanafikra huyo ameongeza kuwa, mbali na ulimwengu wa Kiislamu, barua hiyo inatoa nafasi nzuri ya mazungumzo na ushirikiano miongoni mwa mataifa mbalimbali duniani kwa misingi ya kuheshimiana.

Ikumbukwe kuwa, Kiongozi Mudhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu tarehe 29 mwezi uliopita wa Novemba aliwaandika barua vijana wa Magharibi na kusema kuwa, alipata msukumo wa kuandika barua hiyo kufuatia matukio machungu ya kigaidi hasa ya mjini Paris Ufaransa ya tarehe 13 mwezi uliopita.

Barua hiyo ambayo ni ya pili kwa vijana wa Magharibi baada ya ile ya mwezi Januari imeendelea kuakisiwa kote duniani huku wasomi, vijana na wanaharakati wakisema imekuja wakati unaofaa kwani hivi sasa kumeenea chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za Magharibi pasi na vijana wa nchi hizo kujua ukweli kuhusu Uislamu na Waislamu.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)