Tovuti Hii Imefungwa. Tumehamia Kwenye Parstoday Kiswahili
Jumatatu, 30 Novemba 2015 06:57

Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu (Barua ya Pili)

Radiamali ya AFP kwa barua ya Kiongozi Muadhamu (Barua ya Pili)

Shirika la habari la Ufaransa AFP limetoa ripoti na kusema kuwa, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amewaandikia barua ya pili vijana wa nchi za Ulaya na Marekani na kulaani viwango vya kindumilakuwili vya Magharibi. Shirika hilo limeandika: "Katika barua hiyo iliyosambazwa kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa, Kiongozi wa Iran amesema: Mtu yeyote mwenye mapenzi na ubinadamu huathirika na kuumia anapoona jinai za kigaidi, ni sawa tu jinai hizo ziwe zinatokea Ufaransa, au Palestina, au Iraq, au Lebanon au Syria." Shirika hilo limeendelea kuandika: "Kiongozi wa Iran amelaani siasa zinazogongana za Marekani katika kuanzisha, kulea na kuyapa silaha makundi kama al Qaida, Taliban na makundi mengine ya kigaidi na kusisitiza kuwa, leo hii ugaidi ni machungu yetu sote." Inafaa kukumbusha hapa kwamba, jana, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu aliwaandikia barua ya pili vijana wa nchi za Magharibi. Barua hiyo imetarjumiwa kwa lugha mbalimbali hai duniani, ikiwemo lugha ya Kiswahili na inapatikana katika mtandao wetu wa Intaneti wa kiswahili.irib.ir. Maelezo zaidi kuhusu barua hiyo mtayasikia baada ya taarifa hii ya habari.

Andika maoni


Msimbo salama (Security code)
Upyesha (Refresh)